Umoja wa Mataifa na ustawi wa wanawake DRC

26 Disemba 2016

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake nchini humo MONUSCO pamoja na jukumu la ulinzi wa raia na kusimamia amani, unawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi. MONUSCO, mathalani pamoja na kusaidia wanawake wanaokumbwa na vitendo vya ubakaji, inaenda mbali zaidi na kuwapatia miradi ili waweze kujikwamua na kurejea katika maisha ya kawaida kiuchumi. Je wanafanya nini? Ungana basi na Amina Hassan katika jarida hili maalum akiungana na Langy Stanely wa radio washirika Umoja kutoka Fizi, huko Jimbo l aKivu Kusini nchini DRC.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter