Theluthi moja ya wanaosafirishwa kiharamu ni watoto- Ripoti
Takribani theluthi moja ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu ni watoto, imesema ripoti iliyotolewa hii leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti uhalifu na madawa ya kulevya, UNODC.
Akiwasilisha ripoti hiyo inayoangazia uhusiano kati ya biashara haramu ya binadamu na migogoro, Mkurugenzi Mkuu wa UNDOC Yury Fedotov ameongeza kuwa asilimia 71 ya wahanga wa biashara hiyo ni wanawake na wasichana wanaotumbukizwa kwenye ndoa za lazima na utumwa wa kingono.
Amesema kwa wanaume na wavulana, wao wanaingizwa kwenye ubawabu na sekta ya madini huku na hivyo ameta wanachohitaji kufanya mwaka 2017..
(Sauti ya Fedotov)
“Tunahitaji kusaka njia za jinsi ya kujumuisha nchi wanachama kwenye ushirkiano bora zaidi kwenye kushughulikia changamoto hii kubwa zaidi ya uhusiano pindi fedha haramu kutoka wafanyabiashara ya madawa ya kulevya, wezi wa turathi na wafanyabiashara za binadamu zinapotumika kufadhili ugaidi na misimamo mikali.”
Kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi kubwa ya wahanga wa biashara haramu ya binadamu ni kutoka nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, Amerika ya Kati na Karibea.