Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya kunusurika kwa Boko Haram, Firdau alenga kusaidia watoto

Baada ya kunusurika kwa Boko Haram, Firdau alenga kusaidia watoto

Jimbo la Borno, Kaskazini mashariki mwa Nigeria ni eneo lililoathirika zaidi kufuatia machafuko ya kundi la Boko Haram yaliyoanza karibu miaka miwili iliyopita. Mgogoro huo umesababisha wananchi wengi kupoteza makazi, miongoni mwao ikiwa ni watoto na wasichana wengi wakitekwa nyara na wapiganaji wao.

Kulingana na takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, watoto millioni 28 wamepoteza makazi kutokana na vita na vurugu kote ulimwenguni.

Katika makala hii, tunakutana na msichana Firdau, mwenye umri wa miaka 17, ambaye aliweza kutoroka na kufika kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani, Maidunguri, akielezea yale aliyopitia. Ungana na Selina Jerobon kwa undani zaidi.