Skip to main content

LRA, Boko Haram kikwazo cha amani Afrika ya Kati: UM

LRA, Boko Haram kikwazo cha amani Afrika ya Kati: UM

Kaimu Katibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Afrika ya Kati UNOCA Lounceny Fall amewasilisha ripoti ya Katibu Mkuu mbele ya baraza la usalama kuhusu hali ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR akisema ingawa mchakato wa mpito ulikuwa wa amani, mapigano ya hivi karibuni ni kielelezo cha kuzorota kwa eneo hilo.

Amesema mapigano hayo yaliyokatili maisha ya watu wengi na kusambaratisha wengine yanatokana na tishio kubwa linaloletwa na uwepo wa makundi ya waasi katika ukanda huo

Fall ameliambia baraza la usalama kuwa miongoni mwa vikundi hatarishi ni waasi wa Lord’s Resistance Army LRA la nchini Uganda na kundila kigaidi la Boko Haram,  ambayo yanatakeleza uhalifu nchini CAR na ukanda mzima kwa ujumla.

Amesema kushinda vita hiyo inayovuka mpaka kunahitaji mkakati na kutoa wito.

(SAUTI FALL)

‘‘Nawataka wadau wote kusalia katika kujihusisha na mapambano kisiasa, kifedha an kijeshi ikiwamo kupitia ufadhili wa mipango ya usaidizi wa kibinadamu katika maeneo ambayo LRA imeyaathiri.’’