Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gambia kuendelea kushikilia waandishi wawili inatuatia hofu:UM

Gambia kuendelea kushikilia waandishi wawili inatuatia hofu:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa hofu na kitendo cha serikali ya Gambia kuendelea kuwashikilia rumande waandishi wa habari wawili baada ya wiki mbili tangu kutiwa ndani bila fursa yoyote ya kuonana na familia zao wala mawakili.

Momodou Sabally, mkuu wa kituo cha Radio na televisheni ya Gambia na Bakary Fatty,ripota wa kituo hichohicho, waliswekwa kizuizini na shirika la upelelezi la taifa mjini Banjul tangu Novemba 8 na hakuna mashtaka yaliyoweka dhidi yao.

Mwandishi mwingine ambaye alikamatwa Novemba 10 aliachiwa huru baada ya siku sita bila mashitaka yoyote. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa ameongeza

(SAUTI YA RUPERT)

“Katika kuelekea uchaguzi wa Rais Desemba mosi ni muhimu sana kwamba haki za uhuru wa kujieleza , kukusanyika kwa amani na kujumuika uheshimiwe.”