Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majanga ya asili yagharimu uchumi na jamii- Ripoti

Majanga ya asili yagharimu uchumi na jamii- Ripoti

Benki ya dunia imesema madhara ya majanga ya asili ya kupindukia husababisha hasara ya dola bilioni 520 kila mwaka.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya benki hiyo kuhusu kupunguza athari za majanga ulimwenguni, ikieleza kuwa madhara hayo pia hutumbukiza watu milioni 26 kwenye umaskini kila mwaka.

Akigusia ripoti hiyo kwenye mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, huko Marrakesh, Morocco, Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim amesema majanga hayo yanatishia kufuta mafanikio yaliyopatikana miongo iliyopita katika kutokomeza umaskini.

Amesema vimbunga, mafuriko na ukame vina madhara makubwa kiuchumi na mara nyingi waathirika ni watu maskini.

Kwa mantiki hiyo amesema kujenga mazingira ya kukabili na kuhimili madhara hayo yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi siyo tu ni jambo bora kiuchumi bali pia ni jambo jema kimaadili.

Ripoti hiyo inatokana na utafiti uliofanyika katika nchi 117 ikipendekeza sera bora za tabianchi zitakazolinda watu maski