Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya nyuklia yaongezeka duniani:IAEA

Matumizi ya nyuklia yaongezeka duniani:IAEA

Nchi nyingi duniani hivi sasa zinageukia nyuklia kama chanzo cha nishati amesema mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA.

Akiwasilisha ripoti yake kwenye bodi ya magavana mjini Vienna mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano amesema fursa ya nguvu za nyuklia kwa nchi zinazoendelea isibanwe. Iwezeshwe kupatikana kwa nchi zinazoendelea ili iwasaidie kukidhi mahitaji yao yanayoongezeka ya nishati. Bwana Amano amesema mwaka 2010 ulikuwa wa matumaini kwa upanuzi wa wigo wa nishati ya nyuklia.

Amesema kulikuwa na vinu 66 vilivyokuwa vikijengwa duniani kote na hiyo ni ishara kwamba nguvu za nyuklia zinakuwa na kuendelea kukubalika kimataifa kama chanzo cha nishati salama na kwamba ikitumika vyema itasaidia kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Na amesema pia itapunguza kwa kiasi kikubwa matatizo ya nishati katika miaka ijayo.