Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sayansi ina mchango mkubwa kwa amani na maendeleo:UNESCO

Sayansi ina mchango mkubwa kwa amani na maendeleo:UNESCO

Siku ya kimataifa ya sayanyansi kwa ajili ya amani na maendeleo inaainisha umuhimu wa sayansi katika jamii na kwamba kuna uhusiano mkubwa baina ya sayansi, amani na maendeleo.

Siku hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka Novemba 10, inasisitiza haja ya kushirikisha jamii katika mjadala wa masuala ya kisayansi yanayoibuka na umuhimu wake katika maisha ya watu ya kila siku.

Katika ujumbe maalumu kwa jili ya siku hii mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, Bi Irina Bokova amesema lengo ni kuhakikisha wananchi wapata taarifa kila wakati za maendeleo ya sayansi.

Pia amesema siku hii inahimiza jukumu kubwa walilonalo wanasayansi katika kuelewa dunia yetu na changamoto zake katika kuzifanya jamii hizo kuwa endelevu.