Baraza la usalama kupitisha azimio dhidi ya uharamia Somalia.

Baraza la usalama kupitisha azimio dhidi ya uharamia Somalia.

Baraza la usalama linatarajiwa kupitisha azimio la kuunga mkono hatua zinazochukuliwa na Somalia dhidi ya uharamia, azimio ambalo linakwisha muda wake hapo kesho.

Kwa mujibu wa taarifa ya baraza hilo, Marekani iliandaa azimio ambalo linahuisha hatua dhidi ya uharamia pasina ya mabadiliko makubwa.

Ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali ya uharamia na uhalifu wa kutumia silaha baharini na katika pwani ya Somalia ilichapishwa mnamo Oktoba 7, imesema taarifa ya baraza la usalama.

Katika taarifa hiyo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amekaribisha hatua madhubuti zilizochukuliwa na Somalia na jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na uharamia hususani kuzuia mashambulizi dhidi ya m