Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huu ni wakati wa historia Afghanistan: UM

Huu ni wakati wa historia Afghanistan: UM

Ni wakati wa kihistoria kwa Afghanistan, amesema mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo  Ján Kubiš  wakati taifa hilo likiwa katika mchakato wa kura ya rais na majimbo jumamosi hii.

Bwana Kubiš s ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA amesema licha ya hali mbaya ya hewa pamoja na vitisho lakini wananchi wa Afghanstan wamejitokeza kupiga kura hatua ambayo ameielezea kama kuachiana madaraka kwa njia ya kidemokrasia.

Akiongea na waandishi wa habari nje ya kituo cha kupigia kura mjini Kabul Bwana Kubiš amesema ana matumaini uchaguzi huu utafungua ukurasa mpya kwa nchi.

(Sauti Kubiš)

Huu ni wakati muhimu sana kwa Afghantsan na ningependa kuwapongeza watu wa taifa hili kwa wakati huu wa kihistoria na nimefarijika sana na kuguswa na watu wa Afghanstan. Kwasababu sasa tunapokea taarifa , licha ya kwamba ni mapema sana kusema lolote lakini watu wengi wameonyesha nia ya kupiga kura, wamepanga mistari kila sehemu nchini.

 Huu ni uchaguzi wa kwanza nchini humo unaofanyika chini ya mamlaka ya Afhanstan. Ijumaa waaandishi wa habari wawili walifyatuliwa risasi na kusababisah kifo cha mmoja huku mwingine akijeruhiwa katika  shambulio ambalo UNAMA umelilaani na kuliita la kuchukiza.

Shambuliohilolinafuatia mashambulizi mengine ambayo yalilenga vifaa vya uchguzi mjiniKabulna katika miji mingine nchini  humo.