Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya nyuklia kusaidia kukabili magonjwa ya moyo.

Teknolojia ya nyuklia kusaidia kukabili magonjwa ya moyo.

Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kuwa asilimia 75 ya vifo katika nchi zinazoendelea inatokana na magonjwa ya moyo , na katika juhudi za kuyakabili magonjwa hayo,WHO inashirikiana na shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA. John Kibego na taarifa zaidi.

( TAARIFA YA KIBEGO)

IAEA imafanya mkutano mjini Vienna Austria, na kujaidili matumizi ya nyukilia katika kuchunguza magonjwa ya moyo na hivyo kubaini tatizo mapema.

Wataalamu wa afya kutoka sehemu mbalimbali duniani wametumia fursa ya mkutano huo kubonga bongo kuhusu namna teknolojia hiyo inavyoweza kusaidia kukabili magonjwa ya moyo ambayo mwaka 2012 yaliua takribani watu milioni 17.

Diana Paez ni mkuu wa dawa za nyukilia na uchunguzi katika IAEA.

( SAUTI DIANA)