Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoto yangu ni kuwa Rais wa Somalia- Samira

Ndoto yangu ni kuwa Rais wa Somalia- Samira

Mshauri wa masuala ya vijana na jinsia kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu nchini Somalia, Samire Hussein Duale amesihi wanawake nchini humo kuendelea kusimama kidete ili haki zao zizingatiwe.

Samira, ambaye alizaliwa Kenya lakini amerejea Somalia mwaka 2014 amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kuzingatia changamoto za kiuchumi na kisiasa zinazokabili wanawake nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, mwanaharakati huyo kijana ametaja miongoni mwa masuala muhimu ni uwiano wa uwakilishi akisema ni muhimu ili wanawake wawe sehemu ya mchakato wa kisiasa na upitishaji wa uamuzi.

Amesema wanawake ni watu waaminifu kwenye jamii zao na ni wachapa kazi hivyo kuwa na mwanamke rais, mbunge au waziri bila shaka kutasongesha Somalia, halikadhalika nchi hiyo kuwa chachu kwa mataifa mengine ya Afrika.

Samira amesema licha ya wadhifa wake alio nao hivi sasa, ndoto yake ni kuwa Rais wa Somalia.