Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 71 ya Umoja wa Mataifa na ustawi wa wote

Miaka 71 ya Umoja wa Mataifa na ustawi wa wote

Umoja wa Mataifa hii leo unaadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema ni kipindi cha mpito siyo tu ndani ya chombo hicho bali ulimwengu kwa ujumla. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Katika ujumbe wake Ban amesema miaka 71 inaadhimishwa kukiwa na ajenda 2030 inayolenga kutokumwacha nyuma mtu yeyote, malengo 17 yakipigiwa chepuo, na kwamba ni zama za uendelevu kwa binadamu.

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, maadhimisho yametambua nafasi ya Umoja wa Mataifa kama anavyoelezea msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo Florence Marshall..

(sauti ya Florence)

“Kuhifadhi amani ni jambo muhimu hapa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na ni lazima tuangalie malengo ya maendeleo endelevu na jinsi yatakavyoendeleza kila mtu, hivyo kwa kuwa kila mtu anataka kuishi maisha bora ulimwenguni."

Huko Tanzania, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo, umehamasisha vijana kuingia kwenye kilimo ili kuboresha maisha yao, Jane Michael kutoka Umoja wa Wanavyuo mkoani Dodoma ni shuhuda..

(Sauti ya Jane):