Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM aonya dhidi ya kubana asasi za kiraia Misri

Mtaalamu wa UM aonya dhidi ya kubana asasi za kiraia Misri

Mwakilishi maalumu wa uhuru wa kujumuika na kukusanyika kwa amani Maina Kiai, ameonya leo kuhusu kuongezeka kwa vikwazo dhidi ya asasi za kiraia nchini Misri na kuwalenga watetezi wa haki za binadamu na mashirika ya haki za binadamu.  UN Photo/Jean-Marc Ferré

Tarehe 17 ya mwezi uliopita mahakama ya jinai mjini Cairo ilizuiamali za watetezi tano maarufu wa haki za binadamu na mashirika matatu yasiyo ya kiserikali yaani NGOs tatu zilizotajwa kwenye kesi nambari 173 ya ufadhili wa fedha za kigeni. Uamuzi huo wa mhakama unazeiweka mali hizo chioni ya usimamizi wa serikali , hii ikimaanisha kwamba mashirika na watu binafsi hawawezi tena kufanya maamuzi huru kuhusu fedha zilizozuiliwa.

Bwana Kiai ansema maendeleo haya mapya yanaingilia muktada wa kuwasaka watetezi wa haki za binadamu na mashirika ya asasi za kiraia unaoendelea nchini Misri tangu kufunguliwa kwa kesi dhidi ya NGO mwaka 2011 inayojulikana kama kesi 173 ya ufadhili wa kigeni ambapo watetezi wa haki za binadamu na wakuu wengi wa mashirika ya asasi za kiraia wanachunguzwa.

Amesema hii inaonyesha kwamba serikali inaziandama na kuzilenga asasi za kiraia katika juhudi za kuzima sauti zao. Ametoa wito kwa serikali ya Misri kusitisha mara moja vitendo hivyo na kuhakikisha kwamba inazingatia sheria na viwango vya kimataifa kuhusu NGO’s.