Tuzo ya Sasakawa kutambua upunguzaji wa maafa ya vifo katika majanga:

10 Oktoba 2016

Majina kwa ajili ya uteuzi wa tuzo ya Sasakawa kwa mwaka 2017 yameanza kupokelewa na majaji wanachokitaka ni kutambua mtu binafsi, shirika au mradi ambao umechangia pakubwa katika kuokoa maisha na kupunguza idadi ya vifo katika majanga. Mwisho wa uwasilishaji wa majini ni Januari 31 mwaka 2017.

Robert Glasser, ambaye ni mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la upunguzaji hatari ya majanga UNISDR amesema upunguzaji wa vifo vitokanavyo na majanga ndio kipaumbele , licha ya juhudi zilizofanyika katika maiaka 10 iliyopita kutokana na kuboreshwa na mifumo ya utoaji tahadhari na mipango ya kujiandaa kukabiliana na majanga hayo.

Ameongeza kuwa matetemeko ya ardhi na mabadiliko ya hali ya hewa vimeendelea kukatili maisha ya maelfu ya watu hususani jamii masikini.

UNISDR inasema katika miaka 20 iliyopita watu milioni 1.35 wamepoteza maisha kutokana na majanga.

Tuzo ya Sasakawa inaandaliwa kwa ushirikiano wa UNISDR na mfuko wa Nippon , na huambatana na fedha taslim dola 50,000 kwa mshindi au washindi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter