Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wabunge unaongezeka: IPU

Ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wabunge unaongezeka: IPU

Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wabunge walioteswa na pia ukiukaji wa haki zao za msingi katika mwaka wa 2016 , ambapo kote duniani kuna hatari ya wabunge wanakabiliwa na kunyimwa haki zao za uhuru wa kujieleza, hii ni kwa mujibu wa takwimu za muungano wa mabunge duniani IPU

Takwimu hizo zimetolewa katika kuelekea siku za haki za binadamu ambayo huadhimishwa kila mwaka Desemba 10. IPU imeelezea kuhusu unyanyasaji wa wabunge dhidi ya haki zao ambao umeongezeka kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Mwaka 2016, kamati ya IPU ilichunguza maslahi  ya wabunge 459 kutoka nchi 42 ikilinganisha na wabunge 320 kutoka nchi 43 mwaka 2015, na wabunge 311 kutoka nchi 41 mwaka 2014.  Wabunge walioathirika wanatoka kote duniani ikiwemo 155 wabunge kutoka Amerika (34%), 110 kutoka Asia (24%), 89 kutoka Afrika (19%), 63 kutoka Ulaya (14%), 39 kutoka Mashariki ya Kati na Afrika kaskazini (8%), na 3 (1%) kutoka Kusini mwa Pasifiki.  Na asilimia 73%  ya wabunge hao ni kutoka vyama vya upinzani .

IPU katika kikao chake cha 135 mwezi Oktoba imekitumia kujenga ufanisi na kutekeleza taratibu ya kuhakikisha wabunge wanaweza kwa hiari kujieleza bila hofu ya ghasia, ikiwa ni pamoja na kuheshimiwa kwa kanuni ya kinga ya bunge.