Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto za maji duniani zinaongezeka:Ban

Changamoto za maji duniani zinaongezeka:Ban

Changamoto za maji zinazoikabili jumuiya ya kimataifa zinaongezeka. Changamoto hizo zinachangiwa pakubwa na ongezeko la idadi ya watu duniani, mvua zisizotabirika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, majanga ya mara kwa mara na uchafuzi wa mazingira.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon akizungumza katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu maji kandoni mwa mjadala wa baraza kuu hii leo.

Amesema sababu hizo zinachangia kufanya maji kuwa adimu na hivyo kuweka hatarini juhudi za kupunguza umasikini na kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s. Hivyo akashauri kwamba hatua dhidi ya masuala ya maji inahitajika haraka katika ngazi zote, endapo dunia itaendelea katika mwenendo huu utabiri unaashiria kwamba dunia itakabiliwa na upungufu wa maji asilimia 40 ifikapo 2030.

Ameongeza kuwa lengo nambari 6 la SDG’s kuhusu maji na usafi ni muhimu sana kwa ajili ya kupunguza umasikini na kufikia malengo ya maendeleo endelevu.