Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nuru yaangazia mkataba wa Paris

Nuru yaangazia mkataba wa Paris

Harakati za kufanikisha kuanza kutekeleza mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi zimeongezewa chepuo hii leo baada ya mataifa mengine 31 kutia saini mkataba huo na hivyo kufikia idadi ya nchi 55 zinazotakiwa. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Nats..

Sauti za viongozi mbali mbali mwanzoni mwa mkutano kuhusu uwasilishaji nyaraka za azma ya kutekeleza mkataba wa Paris.. Wanasema watakuwa wameridhia mkataba wa Paris ifikapo mwishoni mwa mwaka huu..

Nats..

Mkataba huu utaanza kutekelezwa iwapo nchi zitakazokuwa zimeridhia ziwe zinachangia asilimia 55 ya hewa chafuzi duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akasema..

(Sauti ya Ban)

“Hakuna muda wa kupoteza. Siku ya leo inatusogeza karibu na kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa Paris mwaka huu. Napongeza nchi 29 zinazochangia asilimia 40 ya uchafuzi kwa kujiunga na mkataba huu.”

Naye Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema serikali zinachukua hatua, sasa ni wadau mbali mbali kusaidia kufanikisha akisema..

(Sauti ya Kerry)

“Nina uhakika tutawezesha mkataba huu kuanza kutekelezwa mwaka huu.”