Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ni changamoto ya haki ya kiraia kwa kizazi hiki:Brown

Elimu ni changamoto ya haki ya kiraia kwa kizazi hiki:Brown

Elimu imeelezwa kuwa ni changamoto ya haki ya kiraia katika kizazi hiki, na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya elimu ya kimataifa.

Gordon Brown ameyasema hayo kabla ya uzinduzi wa ripoti yenye lengo la kutoa mkakati wa kufikia fursa ya elimu sawa kwa watoto na vijana kokote waliko duniani.

Ripoti hiyo ambayo imezinduliwa leo Jumapili inasema kimataifa watoto milioni 263 na vijana hususani waliko Kusini mwa Asia na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara hawaendi shule.

Gordon Brown anaongoza tume ya kimataifa ya ufadhili wa fursa za elimu , mradi ambao unatarajiwa kubadilisha hali ya elimu.

(SAUTI BROWN)

"Mahitaji ya elimu ni mapambano ya haki ya kiraia kwa kizazi chetu. Hadi pale tutakapotafuta njia ya kuzuia wasichana kuolewa mapema wakati ambapo wanahitajika kuwa shuleni, wavulana na wasichana kushinikizwa kuingia katika ajira ya watoto, wakati wanahitaji kuwa shuleni , usafirishaji haramu na wasichana kukataliwa haki zao kwa sababu tu ni wasichana , basi tutakuwa tunakiangusha kizazi chote hiki cha vijana

Brown leo anawakilisha ripoti yake ya kwanza kwa Umoja wa Mataifa.Ripoti hiyo itatafuta mbinu mpya za mtazamo wa ufadhili wa elimu na italenga kujenga utashi wa kisiasa kote duniani ili kupata msaada zaidi wa elimu.

Ripoti inasema kimataifa dola bilioni 39 zitahitajika kwa mwaka hadi 2030 ili kufadhili elimu.