Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwenye uvuvi ziwe fursa- FAO

Changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwenye uvuvi ziwe fursa- FAO

Sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki zikionekana muhimu katika kubadili uchumi wa Afrika, hatua zaidi zinahitajika ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na uvuvi haramu kwa bahari na jamii zinazoishi kanda za pwani.

Ni ujumbe wa mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva  kwa washiriki wa mkutano wa mawaziri wa Afrika kuhusu uchumi utokanao na bahari na mabadiliko ya tabianchi unaofanyika nchini Mauritius.

Da Silva amesema bahari zilizo salama na zenye mazao bora ni muhimu katika kupambana na umaskini vijijini, kuhakikisha upatikanaji wa chakula, kuboresha lishe na kutokomeza njaa.

Hivyo amesema wadau katika sekta za uvuvi, usafirishaji baharini, nishati na utalii wanahitaji suluhu bunifu katika kubadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kuwa fursa.