Kamanda mpya wa UNFIL afanya mkutano wake wa kwanza

25 Agosti 2016

Kamanda na Mkuu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, Meja Generali Michael Beary leo ameongoza mkutano wake wa kwanza kwa pande zote tatu na viongozi waandamizi.

kutoka Jeshi la Lebanon na ofisi ya ulinzi ya Israeli katika Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Ras Al Naqoura. Majadiliano hayo yamehusisha masuala yanayohusiana na utekelezaji wa mamlaka ya UNIFIL chini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa azimio nambari 1701 (2006) kuhusu ukiukwaji huko Blue Line kama vile suala la uondoaji wa majeshi ya Israeli kutoka kaskazini mwa Ghajar.

Meja Jenerali Beary amesema amefurahishwa na mkutano huo na maneno yao ya uamuzi wa kudumisha amani na utulivu lakini pia dhamira yao ya kwenda sanjari na azimio hilo nambari 1701.

Na katika eneo la mashamba ya Shab'a, kusini mwa mstitari wa bluu ambayo yamesababisha hali ya wasiwasi katika eneo la kaskazini mwa msitari huo, amehimiza pande zote kuzuia hali ya

mvutano na uwezekano wa hatari dhidi ya ardhi. Ametoa wito kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuhatarisha utulivu na utulivu wa eneo hilo.

Ameziomba pande zote kutumia zaidi Ofisi yake ya UNIFIL, ili kuweza kusonga mbele akisema, “Anaamini kwa dhati kuwa kuna fursa kubwa ya kuhifadhi utulivu kati ya pande zote katika eneo hilo”.

Ameutaja mkutano huo kuwa wa historia na akasisitiza moyo huo udumishwe.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter