Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shehena ya misaada kwa wakimbizi wa Syria yaondoka Dubai: UNHCR

Shehena ya misaada kwa wakimbizi wa Syria yaondoka Dubai: UNHCR

Shehena kubwa zaidi ya misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wakimbizi wa Syria kuwahi kusafirishwa na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa mwaka huu imeondoka Dubai, Falme za kiarabu Alhamisi. Shehena hiyo ikiwa na vifaa kama vile mablanketi kwa ajili ya watu Laki moja, vifaa vya jikoni zaidi ya seti Elfu Ishirini na Saba na vinginevyo vitasaidia watu zaidi ya Laki Moja na Elfu Ishirini nchiniSyria. UNHCR inasema shehena hiyo inasafirishwa kwa malori 33 na yatavuka mpaka wa Falme za kiarabu hadiJordanna baadaye kusambazwa nchiniSyria. Amin Awad, afisa wa UNHCR hukoAmman,Jordanamesema shirikahilolinafanya kazi ndani yaSyriana nchi jirani kusaidia waliolazimika kukimbia makwao kutokana na mapigano. Mwaka huu pekee, UNHCR imeshasambaza vifaa muhimu zaidi ya wakimbizi wa ndani Milioni Moja na Nusu nchini Syria.