Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Amerika wanaruka jivu na kukanyaga moto:UNICEF

Watoto Amerika wanaruka jivu na kukanyaga moto:UNICEF

[caption id="attachment_292775" align="alignleft" width="350"]dailynews168d-16

Kila mwezi, maelfu ya watoto kutoka Amerika ya Kati wanakabiliwa na hatari ya kutekwa nyara, kunajisiwa na kuuawa wakiwa wanatorokea Marekani kuepuka umaskini na ghasia za vikundi vya kikatili.

Hii ni kwa mujibu ya ripoti iliyotolewa hii leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF). Wengi wa watoto hao wanatoka nchi za El Salvador,Guatemala na Honduras.

Ripoti hiyo inasisitiza kuwa mwaka wa 2014 pekee zaidi ya watoto 44,500 waliokuwa bila wazazi walikamatwa mpakani huku mwaka 2015 idadi ilikuwa karibu watoto 26,000. Ripoti hio inaongezea kuwa watoto hao wasio na wazazi ambao pia wanajikuta bila mawakili wakifapo Marekani asilimia karibu 40 wako katika hatari ya kurejeshwa walikotoka kwenye mazingara magumu.