Skip to main content

Serikali ya Sudan Kusini na SPLM-IO waheshimu usitishaji uhasama:UNMISS

Serikali ya Sudan Kusini na SPLM-IO waheshimu usitishaji uhasama:UNMISS

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini(UNMISS) umerejelea wito wake kwa serikali na kundi la upinzani la SPLM nchini humo kuelekeza nguvu zao katika utekelezaji wa muafaka wa usitishaji uhasama uliofikiwa hivi karibuni kufuatia mapigano yaliozuka Juba.

Kwa mujibu wa Bi Yasmina Bouziane, afisa mkuu wa mawasiliano wa UNMISS, fursa huru kwa wahudumu wa misaada ni muhimu sana katika kuwafikishia msaada maelfu ya watu wanaouhitaji.

Bi. Bouziane amesisitiza wajibu wa UNMISS nchini humo...

(YASMINA CUT 1)

“Kitovu cha majukumu yetu ni kuwalinda raia , kulinda maeneo ya raia pamoja na ulinzi wa raia kwa ujumla katika maeneo yao na mengine ambapo raia wako hatarini. Nakumbusha kila mtu kwamba tuko hapa kwa ajili ya watu wa Sudan Kusini ili wasiwe katika hali ya kuendelea kuteseka”

Na kwa pandezote za katika uhasama

(YASMINA CUT 2)

“Tunazikumbusha pande zote kunahitajika kuwa na uhuru wa kutembea na fursa nchini kote ili watu wa Sudan Kusini wapate msaada katika maeneo ambako ni lazima.