Skip to main content

Timu ya wakimbizi inayoshiriki Olimpiki yaungwa mkono Brazil

Timu ya wakimbizi inayoshiriki Olimpiki yaungwa mkono Brazil

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaoishi ukimbizini jijini Rio De Janeiro, Brazili wamepata fursa ya kushangilia wakimbizi kutoka nchini mwao wanaoshiriki mashindano ya  olimpiki yanayoendelea nchini Brazil . Joshua  Mmali na taarifa kamili.

( TAARIFA YA JOSHUA)

Nats..

Raia hawa wa DRC wanawashangilia wenzao kutoka nchini mwao ambao ni sehemu ya timu ya wakimbizi inayoshiriki kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo mikubwa duniani.

Wakimbizi hao kutoka DRC ni wacheza judo Yolande Makibe na Popole Misenga ambapo licha ya washiriki hao  kutoshinda Carley Kongo ambaye ni mkimbizi nchini Brazil anasema.

( SAUTI CHARLES)

“Suala kwamba wameshindwa, si hoja kwetu. Suala kwamba wameshiriki ni ushindi mkubwa kwao na kwa wakimbizi wote kutoka DR Congo na wakimbizi wengine duniani kote.”