Skip to main content

Ushirikiano unasaidia ushirikishwaji wa kiraia wa vijana Libya:UNICEF

Ushirikiano unasaidia ushirikishwaji wa kiraia wa vijana Libya:UNICEF

Mchango wa Muungano wa Ulaya wa Euro milioni tatu , utalisaidia shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika mradi wake wa majaribio , unaowalenga vijana nchini Libya. Ufadhili huo utaimarisha jitihada za UNICEF za kuongeza idadi ya vijana wanaojiunga na elimu isiyo rasmi , hifadhi ya jamii, na mipango ya burudani na kiutamaduni.

Pia itasaidia ushiriki wa vijana katika mipango ya ujenzi wa amani nchini kote. UNICEF inasema familia , waalimu, makundi ya vijana, serikali za mashinani, asasi za kijamii na sekta zingine katika jamii watakuwa sehemu ya mradi.