Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yasaidia mikutano kuhusu haki na usalama kwa wanahabari Kenya

UNESCO yasaidia mikutano kuhusu haki na usalama kwa wanahabari Kenya

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limesaidia wanahabari 75 nchini Kenya kushiriki mikutano iliyojadili kuhusu haki na usalama wa wanahabari.

Mikutano hiyo mitatu ilifanyika katika kaunti za Machakos, Mombasa na Nakuru, ikilenga kuwahamasisha wanahabari kuhusu haki zao, na haja ya kuwa na uelewa kuhusu usalama wao kazini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa an UNESCO, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumeongezeka visa vya vitisho na mashambulizi dhidi ya wanahabari nchini Kenya, ambavyo vimevuruga uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa.

Ripoti ya utafiti mpya ulioratibiwa na UNESCO imeonyesha kuwa zaidi ya wanahabari 60 walishambuliwa au kutishiwa kazini nchini Kenya mwaka jana, saba miongoni mwao wakiwa wanawake.