Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashabiki wa michezo ya Olimpiki waaswa kusaidia kuwalinda watoto:UNICEF

Mashabiki wa michezo ya Olimpiki waaswa kusaidia kuwalinda watoto:UNICEF

Mashabiki wa michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya watu wenye ulemavu , wameaswa na kupewa changamoto ya kusaidia kuwalinda watoto. Amina Hassan na maelezo kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Changamoto hiyo ipo katika mradi wa kimataifa uliozinduliwa leo na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wa kuwashirikisha watu katika kazi zake kwa ajili ya watoto.

Mashabiki wa michezo kote duniani wanaweza kushiriki katika michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya walemavu bure kwa kujiunga  na mradi wa UNICEF wa kuchukua hatu uitwao”Team UNICEF Get Active for Children”  ambapo dola 5 zitachangishwa kila mshiriki atakapokamilisha kilometa 5 ama kwa kukimbia au kutembea  kwa miguu au kwa kutumia baiskeli ya magurudumu.

Watumiaji pia wanaweza kujikusanyia alama kadhaa kwa kufanya mazoezi au kujibu maswali kwenye majukwaa mbalimbali ya timu ya UNICEF na atakayepata alama nyingi atashinda safari ya kwenda kushuhudia kazi za UNICEF nchini Brazil.

UNICEF imesema muhimu ni kila mtu kuwa katika hamasa ya michezo na kusaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya kazi za shirika hilo za kuokoa na kulinda maisha ya watoto.