UNODC kusaidia wanaojidunga dawa na wafungwa kukabiliana na homa ya ini

27 Julai 2016

Kulekea siku ya kimataifa ya ugonjwa wa homa ya ini, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC imesema inashirikiana na wadau katika kutoa usaidizi kwa wanaojidunga dawa na wafungwa ambao wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa. John Kibego na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JOHN KIBEGO)

Ikimnukuu Mkurugnzi Mkuu Yury Fedetov, taarifa ya UNODC inasema ugonjwa sugu wa hepatitis unasalia kuwa changamoto kwa mifumo ya afya na wale waougua gonjwa hilo linalodhoofisha.

Kwa mujibu wa Fedetov, watu milioni sita ambao hujidunga dawa kote dunaini, huishi na homa ya ini aiana ya C, huku wengine milioni moja waniojidunga dawa wanaugua aina ya B.

Akisisitiza kuwa homa ya ini aina zote hizo mbili  zina kinga na tiba, amesema tatizo hilo limeshamiri zaidi katika magereza ambamo kwayo theluthi tatu ya wafungwa wenye historia ya kutumia dawa za kulevya wana homa ya ini aina ya C.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter