Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wakimbizi wa Msumbiji waliokuwa Malawi warejea nyumbani: UNHCR

Maelfu ya wakimbizi wa Msumbiji waliokuwa Malawi warejea nyumbani: UNHCR

Idadi kubwa ya wakimbizi wa Msumbiji waliokuwa wamekimbilia Malawi wakihepa mapigano kati ya wafuasi wa Renamo na chama tawala FRELIMO wamerejea makwao.

Zaidi ya watu 11,000 walisaka hifadhi nchi jirani Malawi, ambapo kwa mujibu wa tathimini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini humo,maeneo mengi kama vile Kapise ambayo yalifurika wakimbizi yamesaliwa na wenyeji pekee.

Zidi ya dola milioni moja na nusu ziliwekezwa kuwasaidia wakimbizi hao.

Monique Ekoko ni mwakilishi wa UNHCR Malawi.

( SAUTI EKOKO)

‘‘Somo tulilojifunza ni kwamba wakimbizi au wasaka hifadhi watataka kurejea makwao ikiwa kuna usalama. Hatuwezi kuwalazimisha watu kurejea nchini mwao kama hakuna usalama , kurejea nyumbani ni kwa hiari’