Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yalaani shambulio dhidi ya kambi ya Al Sakam

UNHCR yalaani shambulio dhidi ya kambi ya Al Sakam

Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Iraq, Bruno Geddo, amelaani vikali shambulizi lililofanywa dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Al Salam (au Al-Takia) kusini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, ambalo lilisababisha majeraha kwa watoto kadhaa.

Makombora matatu yalirushwa kwenye kambi hiyo, moja likianguka katikati mwa kambi, na mengine mawili yakianguka kwenye eneo la soko, ambapo watoto wanne walijeruhiwa.

Mwakilishi huyo wa UNHCR amesema wamesikitishwa sana na shambulizi hilo la uoga, ambalo ni la tatu la aina yake dhidi ya kambi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Shambulio jingine lilifanyika mnamo Julai 5, 2016 ambapo watu watano waliauawa, wakiwamo watoto wawili.