Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu ya wakimbizi kutoka Kakuma Kenya yajiandaa kwa Olimpiki:UNHCR

Timu ya wakimbizi kutoka Kakuma Kenya yajiandaa kwa Olimpiki:UNHCR

Kwa mara ya kwanza katika historia ya michezo ya Olimpiki , timu ya wakimbizi itashiriki.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, tarehe 5 Agost wanariadha 10 wakimbizi watakimbia chini ya mwamvuli wa bendera ya Olimpiki.

Wanariadha watano kati ya hao 10 , ni raia wa Sudan Kusini waliokimbia vita kwao na kuweka maskani katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Na wanahamasa kubwa kabla ya kuondoka Kenya kuelekea Brazil ambako watawakilisha mamilioni ya wakimbizi duniani katika michuano hiyo ya Olimpiki mjini Rio de Janiero. Rose Nathike ni mmoja wao

(SAUTI YA ROSE NATHIKE)

Najisikia msisimko sana, hii ni fursa ya kwanza kwa ajili ya wakimbizi kushiriki katika michezo ya Olimpiki na kutupa matumaini, ili nasi tuwahamasishe vijana wakimbizi wenzetu ambao wanasalia katika makambi labda kuendeleza vipaji vyao."