Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na Tsipras wa Ugiriki wajadili changamoto za wakimbizi na wahamiaji:

Ban na Tsipras wa Ugiriki wajadili changamoto za wakimbizi na wahamiaji:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekutana na viongozi wa Uguriki na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo ajenda ya maendeleo yam waka 2030 SDG’s, mabadiliko ya tabia nchi na kubwa zidi ni changamoto kubwa ya wakimbizi na wahamiaji nchini humo.

Akizungumza na waziri mkuu wan chi hiyo Alexis Tsipras mapema leo asubuhi amesema Ugiriki ina mchango muhimu kwa Umoja wa Mataifa hususani kwenye ajenda ya kimataifa na kuwashukuru watu wa taifa hilo kwa kuwa raia wa kimataifa.

Wakizungungumza kwa pamoja na waandishi wa habari mjini Athens Ban amesema mjadala hivi sasa ni changamoto kubwa ambayo Ugiriki inakabiliwa nayo ya kushughulikia mahitaji ya mamilioni ya watu wanaokimbia vita na mauaji makwao.

(SAUTI BAN)

“Napenda kuwashukuru watu wa Ugiriki kwa mshikamano mkubwa na huruma waliyoionyesha wakati wote wa dharuaa hii. Licha matatizo ya kiuchumi mliyonayo, Ugiriki imeonyesha ukaribu mkubwa katika kuokoa maisha. Ugiriki inastahili kutamaniwa, pia inastahili msaada mkubwa kutoka jumuiya ya kimataifa. Ugiriki isiachwe kushughulikia changamoto hii peke yake”

Baadaye leo Ban atakwenda kuzuru Lesbos kushuhudia na kutathimini hli halisi ya wakimbizi na wahamiaji.Amesema ni lazima dunia kushirikiana kwa pamoja kuwalinda watu na kushughulikia chanzo cha kukimbia kwao.