Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akiwa Lesbos, Ban Ki-moon akumbusha wajibu wa dunia kwa wakimkbizi

Akiwa Lesbos, Ban Ki-moon akumbusha wajibu wa dunia kwa wakimkbizi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amezuru kisiwa cha Lesbos Ugiriki Jumamosi ambapo ndio kitovu cha kuwasili wa maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterraneankuingia Ulaya.

Akiwa kisiwani hapo na kukutana na wakimbizi Ban ameikumbusha dunia kwamba inawajibu wa kiutu kwa wakimbizi na wahamiaji hao.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na wakimbizi Ban amesema” Leo nimekutana na wakimbizi kutoka katika maeneo yenye matatizo sana duniani, maisha yao yamekumbwa na jinamizi, na jinamizi hilo halijesha. Lakini hapa Lesbos, wamepata mahali ambapo ni mbali sana na vita na mauaji”.

Katibu Mkuu ameupongeza uongozi wa Ugiriki, watu wa Lesbos na jumuiya ya misaada ya kibinadamu kwa msaada mkubwa kwa wakimkbizi hao tangu walipoanza kuwasili. Amerejelea msimamo kwamba Umoja wa Mataifa unajitahidi kuchagiza msaada kutoka jumuiya ya kimataifa , lakini anatambua kwamba hali ya wakimbizi inazidi kuwa mbaya.

Akiongeza kwamba kila siku duniani kote maelfu ya familia zinaendelea kukimbia nyumba zao. Na kila mwezi watu 450 hupoteza maisha kwenye bahari ya Mediterranean.

Ban anazuru Lesbos kwenye kambi hiyo ya wakimbizi ikiwa ni siku mbili tuu kabla ya siku ya wakimbizi duniani nambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 20.