Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA kuisaidia Mauritius kuwa kitovu cha Afrika kupambana na wadudu wa mazao

IAEA kuisaidia Mauritius kuwa kitovu cha Afrika kupambana na wadudu wa mazao

Kifaa kipya (Irradiator) kilichozinduliwa leo nchini Mauritius kitasaidia kisiwa hicho kuongeza vita vyake dhidi ya wadudu waharibifu wa matunda wanaotishia thamani ya mazao na pia kuzisaidia nchi zingine za Afrika katika kudhibiti wadudu hao wanasababisha hasara kubwa za kiuchumi kwa wakulima.

Kifaa hicho cha gharama ya Euro 238,000 kinachofadhiliwa sehemu na shirika la kimataifa la nguvu za atomic kitaiwezesha Mauritius kuinua uwezo wake zaidi ya mara mbili wa kuitumia njia ya kuwafanya wadudu kuwa tasa (SIT) kama njia ya uzazi wa mpango kwa wadudu hao ili kupungua kuzaliana kwao.

Katika hatua nyingine zainazoungwa mkono na IAEA kuboresha mikakati kama hiyo barani Afrika, Mauritius leo pia imezindua mpango wa kwanza wa mafunzo ya SIT yanatakyokuwa yakifanyika kila mwaka.

Mafunzo hayo ya cheti ya miezi mine yataenda hadi nje ya miapaka ya Mauritius.Kundi la kwanza litajumuisha wanafunzi kutoka Botswana, Burkina Faso, Ghana, Kenya, Madagascar, Mauritius, Morocco, Namibia, Nigeria, Sudan, Tanzania na Zambia.

SIT ni njia iliyothibitishwa kufanya kazi, ya gharama nafuu na inayolinda mazingira ambayo inatumika kote duniani kudhibiti mazalia ya wadudu kama hao wanaoathiri matunda.