Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya mpito Sudan Kusini inaleta nuru- Ladsous

Serikali ya mpito Sudan Kusini inaleta nuru- Ladsous

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa ya mpito nchini Sudan Kusini kunatoa fursa ya kushawishi wakimbizi wa ndani walio kwenye vituo vya hifadhi vya Umoja huo kurejea nyumbani.

Ladsous amesema hayo akihojiwa na Radio Miraya ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS baada yakutembelea maeneo ya Bentiu na Malakal ambako wakimbizi wamesaka hifadhi kwenye vituo vya Umoja wa Mataifa.

(Sauti ya Ladsous)

“Cha kuvutia huko Bentiu ni kwamba, katika miezi minne iliyopita si chini ya wakimbizi wa ndani elfu ishirini na tano wamerejea makwao kuandaa mazao, kupanda mbegu na hilo ni jambo la kutia moyo ambalo tungependa liigwe katika vituo vingine, na hiyo itakuwa ishara ya kwamba kuaminiana kunarejea na hata matumaini kwa maisha ya baadaye.”

Bwana Ladsous akaenda mbali kutoa ujumbe wake kwa wana Sudan Kusini.

(Sauti ya Ladsous)

“Nafikiri matarajio ya utekelezaji wa mkataba wa amani na kuundwa kwa serikali ya mpito ya pamoja , yote haya yanaleta matumaini mengi”