Ban amelaani shambulio la Idlib Syria
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani shambulio la Jumapili mjini Idlib Syria ambalo limetokea kwenye soko la mboga na duka pekee la kuoka mikate kwenye mji huo.
Shambulio hilo la anga limetokea wakati ambao mkataba wa usitishaji mapigano kwa miji mine ukiwemo mji wa Idlib umearifiwa kurejeshwa mwishoni mwa wiki.
Duru za habari zinasema shambulio hilo limekatili maisha ya watu kadhaa wakiwemo wanawake na watoto, na kujeruhi wengine kadhaa.