Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yawataka wahudumu wa afya kunawa mikono ili kupunguza maambukizi

WHO yawataka wahudumu wa afya kunawa mikono ili kupunguza maambukizi

Shirika la afya duniani limewataka wahudumu wa afya kuimarisha usalama wa wagonjwa kwa kuzingatia misingi ya usafi wa mikono ili kupunguza idadi ya maambukizi. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

WHO imetoa wito huo leo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kunawa mikono inayoadhimishwa kila mwaka Mei 5.

Kauli mbiu  katika maadhimisho ya mwaka huu ni maambukizi katika maeneo ya upasuaji, msukumo ukitolewa katika kuhakikisha mikono inasafishwa kuanzia wakati mgonjwa anapowasili hospitalini, wakati wote wa maandalizi ya upasuaji na hudma zote baada ya upasuaji mpaka mgonjwa atakaporuhusiwa kwenda nyumbani.

Shirika hilo linasema maambukizi mengi hutokea wakati vijidudu vinapotoka kwenye mikono ya wahudumu wa afya kwenda kwa

Mona Yassin ni afisa mawasiliano, WHO.

(SAUTI YA Mona)

“Ongezeko kubwa la maambukizi kutokana na kutonawa mikono linashuhudiwa zaidi kwenye nchi za vipato vya kati na chini. Tafiti ziliposaka sababu zilihoji wahudumu wa afya na wakataja sababu kuwa hawanawi mikono kwa kuwa hawana muda wanawahi kumhudumia mgonjwa haraka, au wamesahau au hakuna maji! Lakini sababu zote hizi hazikubaliki.”

WHO inasema usafi wa mikono unaweza kuokoa maisha ya watu milioni 8 kote duniani na WHO imetoa wito wa vituo vya afya kujiunga na kampeni ya “Okoa maisha, nawa mikono.