Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amtangaza atakayekuwa mkuu mpya wa UNEP:

Ban amtangaza atakayekuwa mkuu mpya wa UNEP:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon , baada ya majadiliano na wenyeviti wa kanda wa nchi wanachama, ameliarifu baraza kuu nia yake ya kumteua Erik Solheim wa Norway kama mkutugenzi mtendaji mpya wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa mazingira UNEP.

Bwana Solheim hivi sasa ni mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya shirika kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo (OECD),. Wadhifa huo amekuwa akiushikilia tangu mwaka 2013. Na kuanzia 2007 hadi 2012 alikuwa waziri wa mazingira na maendeleo ya kimataifa wa Norway.

Pia amewahi kuwa waziri wa maendeleo ya kimataifa wan chi hiyo tangu 2005 hadi 2007. Bwana Solheim atachukuwa wadhifa huo kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa sasa Achim Steiner anayemaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa miaka 10.