Skip to main content

Uhuru wa kupata habari unahitaji sheria bora na endelevu

Uhuru wa kupata habari unahitaji sheria bora na endelevu

Ikiwa leo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, kauli mbiu ikiwa Kupata taarifa ni haki yako ya Msingi idai!, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez amesisitiza umuhimu wa uhuru wa tasnia hiyo katika kuwapatia wananchi habari ikiwemo malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku hiyo huko Mwanza, Tanzania Bwana Rodriguez ametaja lengo namba 16 lenye kiashiria kinachopima uhuru wa vyombo vya habari katika kufanikisha jukumu hilo huku Waziri wa Habari Nape Nnauye akiwatoa shaka kuhusu uhuru huo..

(Sauti ya Nape)

Naye Jaji Mkuu wa Tanzania kupitia mwakilishi wake kwenye mkutano huo Jaji Robert Makaramba amesema jukumu la tasnia hiyo ni kusimamia utawala bora na hivyo..

(Sauti ya Jaji Makaramba)