Skip to main content

UNICEF yaalani vikali kutekwa kwa watoto 100 Magharibi mwa Ethiopia

UNICEF yaalani vikali kutekwa kwa watoto 100 Magharibi mwa Ethiopia

Watoto 100 wametekwa nyara Magharibi mwa Ethiopia mwishoni mwa wiki wakati wa shambulio la wizi wa ng’ombe linalodaiwa kufanywa na watu kutoka Sudan Kusini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, limelaani vikali shambulio hilo ambalo limekatili maisha ya watu na kujeruhi wengine wengi. Christopher Boulierac ni msemaji wa UNICEF..

(SAUTI YA BOULERAC)

"Ripoti zinaonyesha kwamba watoto ni miongoni mwa waliouawa na kujeruhiwa, wafanyakazi wetu wanasaidia hali ya watoto walioathirika na kitendo hicho cha kikatili, na wako tayari kusaidia jamii. UNICEF inaungana kutoa wito wa kuachiliwa kwa watoto hao bila masharti na kurejeshwa kwa familia zao”