#UNGASS: Zaidi ya watu 3000 wapata huduma dhidi ya dawa za kulevya Tanzania
Kikao maalum cha siku tatu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu tatizo la dawa za kulevya duniani UNGASS, kimeanza leo mjini New York ambapo wadau watatumia fursa hiyo kuibua mikakati ya kukabiliana na dawa za kulevya kwa mujibu wa maazimio ya baraza hilo. Amina Hassan na taarifa kamili.
Ni kiongozi wa kikao hicho akiwaalika wajumbe kukaa kimya kwa dakika moja kutafakari na kuombea mkutano.
Kisha Rais wa baraza kuu Mogens Lykketoft ambaye ni mwenyeji wa kikao hiki akawakaribisha na kuwahutubia wajumbe akisema..
(SAUTI MOGENS)
‘‘Hakika hili ni tatizo mtambuka . Kutoka haki za binadamu hadi maendeleo endelevu, madhara ya kiafya kwa watumiaji wa dawa za kulevya, na rushwa hadi uhalifu wa kupangwa".

(Sauti ya Dkt. Nyandindi)

Amesema ni lazima kuweka binadamu kwanza, kupitia huduma za afya, kuheshimu haki ya walioathirika na kuzingatia ustawi wa jamii.
Kwenye azimio lililopitishwa leo, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekariri msimamo wao wa kutatua tatizo la dawa za kulevya ili hatimaye kukuza jamii isiyokuwa na dawa hizo.
Miongoni mwa harakati zilizotajwa ni kuhakikisha waathirika wa dawa za kulevya wanapata huduma za dawa zinazowasaidia kupunguza maumivu yao, kuzingatia kinga, kupambana na kilimo na biashara haramu za dawa hizo pamoja na vikundi vya uhalifu wa kimataifa.
Bwana Fedotov pia ametoa wito wa ufadhili akisema hakuna mafanikio yatakayopatikana iwapo maazimio yaliyopitishwa hayatapewa ufadhili unaohitajika.