Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walemavu pia ni watu..Dkt. Florence Wachira-Kenya

Walemavu pia ni watu..Dkt. Florence Wachira-Kenya

Ingawa walemavu ni asilimia ishirini ya watu duniani kote, bado watu hawa huachwa nyuma kwenye masuala ya maendeleo kote duniani. Wakati wa Mkutano wa 60 wa wanawake CSW60 ambao bado unaendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani, maendeleo kwa wanawake na wasichana walemavu ni moja ya mada zilizojadiliwa. Mwenzetu Amina Hassan amefanya mahojiano na Dkt. Florence Wachira ambaye ni Kamishna wa Kamisheni ya Kitaifa ya Usawa wa Jinsia nchini Kenya, akianza kkwa kumuuliza lengo la tume yake hasa katika mkutano huu..