Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa asjili wawezeshwe bila kutegemea serikali wala wanaume zao: CSW60

Wanawake wa asjili wawezeshwe bila kutegemea serikali wala wanaume zao: CSW60

Suala la wanawake wa jamii za watu wa asili limepewa kipaumbele kwenye mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake CSW60 unaoendelea wiki hii mjini New York Marekani, ukimulika mchango wao katika kutokomeza umaskini.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN women, wanawake wa asili wanapaswa kupewa nafasi zaidi katika ngazi zote za uongozi ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye jamii zao.

Akizungumza na Priscilla Lecomte wa idhaa hii, mwakilishi wa jamii za watu wa asili wa Kenya, Valerie Kasaiyian, kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa Mawasiliano wa Watu wa Asili, amesisitiza umuhimu wa kusaidia wanawake kujitegemea, hapa akianza kueleza mtazamo wake kuhusu uwezeshaji huo.