Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili operesheni za ulinzi wa amani,vitendo vya ukatili wa kingono.

Baraza la usalama lajadili operesheni za ulinzi wa amani,vitendo vya ukatili wa kingono.

Baraza la Usalama leo limekutana kujadili operesheni za ulinzi wa amani likiangazia unyanyasaji wa kingono na ukatili. Amina Hassan na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA AMINA)

Mkutano huo ulitawaliwa  na matamako ya kulaani vitendo vya ukatili wa kingono vinavyofanywa na walinzi wa amani ambao wanatakeleza wajibu muhimu wa amani na usalama katika nchi mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa msemaji wa kwanza ambapo amerejelea kile alichokiita saratani akisisitiza kuwa vitendo  hivyo vinakwenda kinyume na maadili yanayosimamiwa na UM.

Ban amesisitiza umuhimu uchunguzi wa haraka ndani ya miezi sita dhidi ya vitendo hivyo, kuchukua hatua dhidi ya walinda amani wanaofanya vitendo  hivyo na kutaka nchi wanachama  kuwafikisha mahakamani raia wao ambao walifanya vitendo hivyo wakiwa wanatumikia Umoja wa Mataifa na akaongeza.

(SAUTI BAN)

‘‘Pia tutazingatia kuweka sheria mpya ya kuwaondoa walinda amani katika shughuli za kijamii ikiwamo maeneo maalum kama  nje ya mipaka’’