Skip to main content

Kujitolea kunaweza kuibua fursa kwa vijana

Kujitolea kunaweza kuibua fursa kwa vijana

Nchini Tanzania leo shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limekuwa na kongamano kuangalia ni kwa jinsi gani vijana wanaweza kushiriki katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na kujikwamua kimaisha, wakati huu ambapo shirika hilo limetimiza miaka 50.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni fursa ya vijana kujikwamua kupitia kujitolea ambayo mtoa mada Fatma Mohammed anayejitolea kupitia UN-Habitat amesema ni dhana ambayo ikieleweka itasaidia vijana kukwamua.

Fatma amemweleza Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa kuwa kujitolea ni katika nyanja zote ikiwemo uhandisi na uandishi wa habari kwa kuwa…

(Sauti ya Fatma)