Skip to main content

FIJI yaomba dola milioni 38.6 kusaidia ukarabati baada ya kimbunga Winston

FIJI yaomba dola milioni 38.6 kusaidia ukarabati baada ya kimbunga Winston

Wawakilishi wa serikali ya Fiji na Umoja wa mataifa leo wamezindua ombi la msaada wa dola milioni 38.6 mjini Geneva ili kutoa msaada muhimu wa dharusa kwa watu 350,000 walioathirika na kimbunga Winston.

Kimbunga hicho kilichokuwa na uharibifu mkubwa katika historia ya ukanda huo, kilikikumba kisiwa cha Fiji usiku wa Februari 20 , kikikatili maisha ya watu 40 na kuathiri wengine 35,000 ikiwa ni asilimi 40 ya watu wote wa kisiwa hicho.

Watu wengine Zaidi ya 54,000 wako katika vituo maalumu hadi sasa. Kwa mujibu wa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA Stephen O’Brien anatoa dola milioni 8 kutoka mfuko wa dharura wa msaada wa Umoja wa mataifa CERF ili kusaidia baadhi ya miradi ya iliyoorodheshwa kwenye ombi la msaada.

Wahisani wa kimataifa wameshatoa msaada wa kiufundi wa thamani ya dola milioni 22 na fedha taslimu milioni 9 kwa ajili ya kisiwa hicho.