Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaonya juu ya zahma ya kibinadamu Ugiriki huku kukiwa na taharuki ya Ulaya kuhusu wahamiaji

UNHCR yaonya juu ya zahma ya kibinadamu Ugiriki huku kukiwa na taharuki ya Ulaya kuhusu wahamiaji

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kwamba Ulaya iko katika hatihati ya zahma kubwa wa kibinadamu.

Na hii ni kutokana na kufurika kwa idadi kubwa ya watu Ugiriki taifa ambalo tayari linalemewa, wakati hakuna ushirikiano unaohitajika kwa serikali zingine licha ya makubaliano katika masuala mbalimbali nan chi mbalimbali zikiweka sheria kali dhidi ya miaka yao.

Shirika hilo limesema hatua zisizona mpangilio zinazidisha madhila kwayasiyo ya lazima na hatari ya ugomvi na muungano wa Ulaya kukiuka viwango vya sheria za kimataifa. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

"Ugiriki haiwezi kuhimili hali hii peke yake, kwa hiyo bado ni muhimu sana Ulaya kutekeleza makubaliano ya uhamiaji walioafikia mwaka jana, yapewe kipaumbele na yatekelezwe , ni lazima iwasikitishe kila mmoja wenu kwamba, mbali na makubaliano ya uhamishaji wakimbizi 66,400 kutoka Ugiriki, mpaka sasa, nchi za ulaya zimeahidi nafasi 1,539  tu, na kati ya hizo mpaka sasa wamehamisha wakimbizi 325 tu ."

Kufikia jana Jumatatu idadi ya wakimbizi na wahamiaji nchini Ugiriki wanaohitaji malazi imeongezeka na kufikia 24,000.