Skip to main content

UNESCO , RFI kupigia chepuo historia ya bara Afrika

UNESCO , RFI kupigia chepuo historia ya bara Afrika

Shirika la Elimu ,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na redio ya kimataifa ya Ufaransa RFI, leo wametiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kihariri wa kupigia chepuo ukusanyaji wa kitabu cha historia ya Afrika.

Taarifa ya UNESCO inasema kuwa katika makubaliano hayo RFI kupitia kipindi chake cha wiki kiitwacho kumbukumbu ya bara kitajikita katika historia ya jumla pamoja na makabiliano dhidi ya chuki inayonyemelea historia ya bara Afrika.

Mfululizo wa vipindi hivyo 52 vinavyoanza tarehe saba Februari, utamulika kumulika kwa mpangilio mada katika kila mwezi kama vile historia ya jumla ya Afrika, kwanini na namna gani, Afrika na asili ya ubinadamu,, ukweli na mbinu pamoja na Afrika ya kale kablaya karne ya saba na maudhui mengineyo.

Mradi huo wa historia ya jumala ya Afrika uliop chiniya UNESCO na ambao ulizinduliwa mwaka 1964, ulilenga kuainisha historia ya bara hilo huru na dhana ya kuzaliwa katika utumwa na ukoloni.