Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni fursa kwa wanawake: Dk Glemarec

Harakati dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni fursa kwa wanawake: Dk Glemarec

Mkuu wa sera na mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake, UN Women Dk Yannick Glemarec amesema kuna fursa ya kupunguza pengo la kijinsia kupitia harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchilicha ya chamgamoto kadhaa kama vile rasilimali fedha, teklnolojia na soko.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa mjini Abu Dhabi kunakofanyika mkutano kuhusu namna nishati mabadala inavyoweza kusaidia athari za mabadiliko ya tabianchi Dk Glemarec amesema wanawake wanaweza kuwezeshwa kukabiliana na tabianchi hususani katika kilimo.

Dk Glemarec hata hivyo ametoa anagalizo.

(SAUTI DK GLEMAREC)

Hatuna muda wa kuchukua hatua, kwasababu mabadiliko ya tabianchi yataongeza vikwazo ambavyo wanawake wakulima wanakabiliana navyo, kwani sio rahisi kupata fedha kwa za mbegu na mbolea pamoaja na mifumo ya umwagiliaji.